GUEST POST

Swahiba nawatamani

Moyo wanipaparika
Nataka kukuambia
Midomo yamebanika
Nimebaki nakulia
Mikono yatetemeka
Najaribu kwandikia
Risala ikitumika
Uisome swahibia

Moyo unasononeka
Nakutamani swahibu
Mwili medhoofika
Mpaka napata tabu
Hata kama wasikika
Bado mie sijatubu
Nahisi huko kufika
Nikupikie kababu

Leo lipi menipata
Mpaka hivi nalia?
Nakumis kama bata
Natamani kukimbia
Ama nipande skuta
Kuja kukusalmia
au niruke ukuta
Swahiba kukwangalia

Si dhihaka nisemayo
Ni huzuni nasikia
Masiku ni hayohayo
Mbio yanajipitia
Sitamani niwe nayo
Mambo yote ya dunia
Ila tabia nijuayo
Yako Farwa nisikia

Kalamu imevunjika
Siez Kuendelea
Na wino watiririka
Kartasini kuingia
Na mimi nahuzunika
Kwaheri kukuambia
Jina langu kitamka
mimi wako farhia

Farhiya zubeir


3 thoughts on “GUEST POST

  1. Awesome

    Liked by 1 person

Leave a comment