WALIMU WETU MAKANDE

Naanza yangu nudhuma,ewe Mola niongoze..Yote nipate yasema, wasojua niwajuze.. Walimu wa sifa njema,heri Mungu awajaze..Heko nawapa pongezi,walimu wetu Makande .

Nimetembea tembea,mabara na visiwani..Ila sijajionea, uzuri uso kifani..Wa walimu wetu hawa, wafunzao kwa makini.. Heko nawapa pongezi walimu wetu Makande.

Ni walimu maridhia,na wa kupendwa na watu..Sifa wamejipatia,kwa uzuri wao utu..Naye mola kawajaalia,mema yasio na kutu..Heko nawapa pongezi,walimu wetu Makande.

Ms Mohammad nikianzia, mwalimu mwenye busara.. Kwenye business kabobea, ywafunza pasi papara.. Tena Mungu namuombea, amuepushe madhila..Heko nawapa pongezi , walimu wetu Makande.

Na Salee naye pia, mwalimu wa kiingereza.. Yeye bidii anatia,Sina budi kumpongeza.. Twampenda nawambia, kimasomo hutuhimiza.. Heko nawapa pongezi ,walimu wetu Makande.

Kwa upande wa kemia,bi Stella aongoza..Na pia kwa fisikia,ni masoni anafunza.. Aidha gografia, kimemia atujuza.. Heko nawapa pongezi,walimu wetu Makande.

Na somo la Kiswahili,pia tunaye mwalimu..Si mwengine Ni meali, mwalimu mwenye nidhamu.. Tunampenda kwa kweli,katu hatuishi hamu.. Heko nawapa pongezi, walimu wetu Makande.

Sikumsahau muteti, mwalimu wa historia..Na somo la hisabati,Ni masoni nawambia.. Wamefanya mikakati,elimu kutupatia.. Heko nawapa pongezi,walimu wetu Makande.

Na pia bwana Makoha, mwalimu mwenye ujuzi..Yeye anafunza lugha,lugha yenye ufunuzi..Tena yenye ufasaha, nao mwingi ufanisi.. Nawambia si mzaha,Yeye Ni mchapakazi .

Nakuomba ya jalali, naomba nami nalia..muhifadhi prinsipali,na shari za kidunia..Ni mwalimu wa kikweli,kufundisha ajulia.. Heko nawapa pongezi,walimu wetu Makande.

Walimu mlosifika, Twawapenda bila shaka.. Twawapenda kwa hakika, shahidi yetu rabuka.. Tena tumefurahika, Makande galzi kufika.. Miaka minne’mekamilika, twazidi kuwakumbuka.

Advertisements

2 thoughts on “WALIMU WETU MAKANDE

  1. Wel done my dia
    …bt tumia sound za kiswahili kama vile jografia….ama jografy…fiziki ama fizikia….vitu ka hvyo
    Na zidi kupanua mawazo enwei good work i love it

    Liked by 1 person

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s