MAISHA YANGU BILA BABA

Bisimilahi ya mannani, kwa jina lako karima..Mola uso na kifani,natanguliza heshima..Kisha kwa tumwa amini,na ahli zake kirama.. Maisha yangu jamani,bila Baba yaniuma.

Nimeketi na mamangu,ndiye baba ndiye mama..Si mwengine bali wangu,nimpendaye halima.. Kutimiza yalo yangu,mambo yake hujinyima.. Maisha yangu jamani,bila baba yaniuma.

Roho yangu huniuma, wengine kuita Baba.. Nimemzoea mama,sijui kuita baba..Moyo wangu hunithoma,kama nlodungwa mwiba.. Maisha yangu jamani,bila baba huniuma.

Babangu sijamuona,tangu alipoondoka..Hadi sasa Ni kijana,hajui nilipofika..’Menifanya Sina mana,mbeleni ‘tanikumbuka.. Maisha yangu jamani,bila baba yaniuma.

Baba kuwaacha wana,Ni nini kama si dhulma..Tena alosoma sana,ajua ovu na jema..Na wala huruma hana,wana kumuachia mama.. Maisha yangu jamani, bila baba yaniuma.

Metaabika mamangu,hakutaka kutuwacha..Menilea na ndu’ zangu,Khalid shery kimapacha..Na Mimi naapa Mungu,mamangu sitomuacha.. Maisha yangu jamani,bila baba yaniuma.

Baba ndiye kiongozi,tena mwenye majukumu..Sharifu hajamaizi, kwamba kwake ni muhimu..Kutekeleza malezi,na tena kuwa na hamu.. Maisha yangu jamani,bila baba yaniuma.

Metufanya Ni yatima, furaha kutukosesha..Nikikumbuka ya nyuma,yalivyokuwa maisha..alivyoteseka mama,ili kutufurahisha.. Maisha yangu jamani,bila baba yaniuma.

Advertisements

10 thoughts on “MAISHA YANGU BILA BABA

 1. maskini😢😢😢😢😢mungu atakupa subra inshaallah

  Liked by 1 person

 2. am sad and happy in equall measure.Allah akupe subra

  Liked by 1 person

 3. Avery touching poem……in shaa Allah he wil get the message and regret his doings….subra in shaa Allah….Allah ma3ana..wonderful sis…..

  Like

  1. Shukran jazilla habibty

   Like

 4. Mashaallah

  Like

 5. Ewe ndugu yangu farwa , sikiza takayo nena
  Usilie sana ngowa ,

  Liked by 1 person

 6. Ewe ndugu yangu farwa , sikiza ninayokwambia
  Usilie sana ngowa , ukamkufuru jalia
  Kwani yeye ayajuwa , kila jambo apangia
  Maisha yako bila baba , yasikunyime furaha

  Shukuru unae mama , alokulea ki hali
  Shida zako kutazama , hakuna wake mithili
  Tokea nyaka za nyuma , yeye ni wako kivuli
  Maisha yako bila baba , yasikunyime furaha

  Mola hakupi kilema , akakukosesha mwendo
  Shida huzipa salama , kilio kaeka kando
  Omba kwa wako karima , uupate mwema mwendo
  Maisha yako bila baba , yasikunyime furaha

  Kwa ukweli yana dhiki , lakini budi hatuna
  Ila nikuyasadiki , kumwelekea rabana
  Kwani yeye ni maliki , ajua zaidi sana
  Maisha yako bila baba, yasikunyime furaha

  Liked by 2 people

  1. Waaaah shukran sana 😊malenga…. Shairi on point 👌nakuvulia kofia👏….N nashkuru kwa faraja pia.

   Liked by 1 person

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this:
search previous next tag category expand menu location phone mail time cart zoom edit close